4x4

TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600,MWANZA

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania
 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600. (PICHA NA MDAU BALTAZAR MASHAKA)

 Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo.
 Diwani wa Kata ya Mkuyuni, ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula , Lugo Fasheni akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti  unaotekelezwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL ), jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. TBL tayari imesaidia kupanda miti 2600 jijini Mwanza.

  Afisa Misitu Jiji la Mwanza, Kaombe Phidelis, akitoa taarifa ya hali ya misitu kwa mgeni rasmi , Henry Mongi wa pili kutoka kushoto,katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jana.Wa kwanza ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria TBL, Steven Kilindo .
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegezi na mtumishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakipanda mti kwa pamoja katika shule hiyo, jijini Mwanza juzi. TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600

0 comments:

Post a Comment