4x4

TBL YAFANIKISHA UPANDAJI MITI 2600,MWANZA

 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania
 Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa TBL, Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600. (PICHA NA MDAU BALTAZAR MASHAKA)

 Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo.
 Diwani wa Kata ya Mkuyuni, ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula , Lugo Fasheni akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti  unaotekelezwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL ), jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. TBL tayari imesaidia kupanda miti 2600 jijini Mwanza.

  Afisa Misitu Jiji la Mwanza, Kaombe Phidelis, akitoa taarifa ya hali ya misitu kwa mgeni rasmi , Henry Mongi wa pili kutoka kushoto,katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jana.Wa kwanza ni Meneja wa kiwanda cha Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria TBL, Steven Kilindo .
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegezi na mtumishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakipanda mti kwa pamoja katika shule hiyo, jijini Mwanza juzi. TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600

NAIBU WAZIRI ANGELLA KAIRUKI NA SCHOOLMATE WAKE WA ZANAKI


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angella Kairuki akishow love na my schoolmate wake Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu katika viwanja vya Mnazi hivi karibuni wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani.

JK AIPATIA TBL TUZO YA MWAJIRI BORA 2012

Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali  Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto cheti baada y kuwa mmoja wa wafadhiri wa hafla ya kuwazawadia waajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
 Mkurugenzi wa Rasilimali  Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto akishangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete kumkabidhi tuzo ya ushindi wa tatu ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kenneth Wanyoto cheti baada y kuwa mmoja wa wafadhiri wa hafla ya kuwazawadia waajiri Bora wa Mwaka 2012 katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
 Wanyoto akipita na tuzo mbele ya Rais Kikwete pamoja na Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige
                        Reynada Sikira wa TBL, akipokea tuzo nyingine waliyoshinda
                            Meza waliyokuwa wamekaa baadhi ya wafanyakazi wa TBL
                                                           Wanyoto (kulia) akiwa na furaha

HAFLA YA WAZIRI DK. MGIMWA KUKABIDHI TUZO WAFANYAKAZI BORA

 
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (kushoto)  akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa (kulia) . Tafrija fupi ilifanyika jana mjini Dar es salaam kufuatia kuchaguliwa kwake mwezi Mei mwaka huu kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2012.
 Mkuu wa Mfuko wa Mikopo wa Hazina kutoka Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali , Wizara ya Fedha Christina Ngonyani (kushoto)  akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa kitengo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ilifanyika jana mjini Dar es salaam kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2012.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto)  akipokea tuzo ya ufanyakazi bora wa Wizara hiyo kutoka kwa Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa(kulia) . Tafrija fupi ya kuwazawadia wafanyakazi bora ilifanyika jana mjini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.

 Waziri wa Fedha Dkt . William Mgimwa (katikati) akiwapongeza wafanyakazi wa Wizara ya Fedha walichaguliwa mwezi Mei mwaka huu kuwa wafanyakazi bora kwa mwaka 2012. Tafrija fupi ya kuwazawadia wafanyakazi bora ilifanyika jana mjini Dar es salaam na kuhudhuriwa na wafanyazi mbalimbali.
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa , Katibu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah wakishirikiana na viongozi wa TUGHE na wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar es salaam kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa tafrija fupi jana ya kuwapongeza wafanyakazi bora  wa mwaka huu. Picha zote na GCU- HAZINA

MKUTANO WA SITA WA MENEJIMENTI YA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Ndg. Justine Mwandu akifungua mkutano wa Sita wa Mameneja wa shirika hilo katika hoteli ya Sea Scape iliyopo maeneo ya Mbezi, Dar es Salaam tarehe 3 Desemba 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bima za Maisha, Bi. Rose Lawa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Anne Mbughuni. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bima za Mali na Ajali, Ndg Ndugu Kura Kalema.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mwandu (kushoto) akiwakaribisha wajumbe katika mkutano. Anayesalimiana nae ni meneja wa bima tawi la Songea Ndugu Moses Senje akifuatiwa na meneja mwenzake tawi la Tanga Ndugu Romanus Hokororo na mwisho meneja wa Iringa Ndg Ally Mohammed.
Kutoka kulia ni Bw. Henry Machoke, Mkurugenzi wa Masoko, akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa NIC, Elisante Maleko, na Meneja wa tawi la Ubungo, Segeja Mabula katika mkutano huo.
akurugenzi pamoja na Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano.

UZINDUZI KAMPENI YA LISHE LINDI

 Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu (kulia) akikabidhi zawadi ya simu ya mkononi kwa mkazi wa Lindi, Asha Mkingamila, ambaye aliweza kueleza vizuri kuliko wengine  nini
maana ya lishe bora , katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Save the Childern Tanzania, Rachel Pounds.
 Mkazi Lindi, Habiba Rashidi, akihamasisha wakazi wa mkoa huo kuhusu umuhimu wa lishe bora wakati wa maandamano ya watoto, katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo
la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni
mwa wiki.
 Baadhi ya watoto wa Lindi wakitembea kwa maandamano katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na
Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki.
 Mkurugenzi wa Shirika la Watoto la Save the Children Tanzania, Rachel Pounds, akizungumza  katika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto ulioandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mratibu wa Lishe katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sarah Mshiu, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Hamidi Nassoro, Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mafuru Mng’ong’o na Mbunge wa Serengeti, Dk Kwebe Stephen Kwebe.
 Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Lediana Mafuru Mng’ong’o, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha umuhimu wa lishe bora yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto ulioandaliwa na Shirika la Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Jukwaa la Lishe Tanzania (PANITA) katika Uwanja wa Ilulu, Mkoani Lindi mwishoni mwa wiki. BURUDANI PIA ZILIKUWEPO, JE UNATAKA KUONA? BOFYA HAPA KWENYE UKURASA WETU WA MICHEZO, BURUDANI NA SANAA