4x4

MWANAFUNZI WA IFM AFARIKI KIFO CHA KUTATANISHA


Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri.
Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni.
Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
Aliyevaa Koti jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.
Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.

Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA SEMINA ELEKEZI YA MASHEIKH WA BARAZA KUU LA WAISLAMU TANZANIA (BAKWATA)MJINI DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akijumuika kuomba dua iliyoombwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba (katikati) baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo, Julai 15, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo, Julai 15, 2012. Katikati ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, baada ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo, Julai 15, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya za Kiislamu wakati akiondoka, baada ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo, Julai 15, 2012.
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya za Kiislamu na waumini wa Dini hiyo, waliohudhuria semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo, Julai 15, 2012. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR

WANAHARAKATI KUTOKA VYUO VYA ELIMU YAJUU WAPINGA MGOMO WA MADAKTARI

 Kundi la wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu nchini, wakiwa na mabango jana katika hospitali ya taifa, Muhimbili, Dar es Salaam, kushinikiza madaktari waache mgomo.
 Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu Abubakari Assenga (kushoto), akiwa na Katibu wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Edwin Chitange, baada ya maandamano ya wanaharakati hao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kusitisha mgomo
 Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya Juu, Abubakar Assenga akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano yao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kuacha mgomo.
 Mwanamke aliyekuwa akisubiri kuona mgonjwa wake, Katika hospitali ya Muhimbuli, Dar es Salaam, Helen Thomas, akisoma bango lililoachwa na wanaharakati hao wa vyuo vya elimu ya juu.
Wanaharakati wa vyuo vya elimu ya juu, wakihanikiza baada ya kufika Muhimbili kutaka madaktari waache mgomo