4x4

MKUTANO WA SITA WA MENEJIMENTI YA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Ndg. Justine Mwandu akifungua mkutano wa Sita wa Mameneja wa shirika hilo katika hoteli ya Sea Scape iliyopo maeneo ya Mbezi, Dar es Salaam tarehe 3 Desemba 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bima za Maisha, Bi. Rose Lawa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Anne Mbughuni. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bima za Mali na Ajali, Ndg Ndugu Kura Kalema.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mwandu (kushoto) akiwakaribisha wajumbe katika mkutano. Anayesalimiana nae ni meneja wa bima tawi la Songea Ndugu Moses Senje akifuatiwa na meneja mwenzake tawi la Tanga Ndugu Romanus Hokororo na mwisho meneja wa Iringa Ndg Ally Mohammed.
Kutoka kulia ni Bw. Henry Machoke, Mkurugenzi wa Masoko, akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa NIC, Elisante Maleko, na Meneja wa tawi la Ubungo, Segeja Mabula katika mkutano huo.
akurugenzi pamoja na Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano.

0 comments:

Post a Comment