4x4

DAKTARI ULIMBOKA ALIPOFIKISHWA MUHIMBILI AKIWA MAHUTUTI BAADA YA KUPIGWA NA WATU WASIOJULIKANA

 Ilibidi usalama kuimarishwa  kwenye eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili muda mfupi kabla ya Mwnyekiti wa Jumuia ya Madaktari Tanzania Steven Ulimbvoka kufikishwa hospitalini hapo lifiatia kipigo alichopata kutoka kwa watu wasiojulikana ambao inadaiwa walimteka  usiku wa kuamkia leo
 Hali ikawa hivi
 Ikawa hata kupiga picha tukio hilo inazuiwa  na polisi waliovalia kiraia kama huyu
 Hata polisi Auxilary wa Muhimbili nao walipata kazi kama huyu (kushoto)
 Mazingira yakawa hivi
 Watu wakkaa makundi makundi kujua kulikoni
 Lango la MOI likiwa limefungwa kabla ya Ulimboka kufikishwa hospitalini hapo kwa kuwa mgomo wa madaktari ulikuwa ukiendelea
 Baadaye lango la MOI likafunguliwa kidoogo  lakini hakuna wagonjwa waliokuwa wakiruhusiwa kuingia, alikuwa anasubiriwa Ulimboka tu.
 Babu  (mwenye msuli) ambaye ni mgonjwa aliyehitaji huduma hakuipata kwa sababu mgomo ulikuwa ukiendelea 
 Kisha Ambulance iliyombeba Ulimboka ikafika Muhimbili
 Wapigapicha wakawa na kazi mshike mshike, kiasi cha baadhi yao kama huyo Tryphone Mweji wa The Cuardian akalazimika kutumia mbinu ya kupanda kwenye majengo hospitalini hapo kupata piocha bora, labda ya mwaka/
 Madaktari licha ya kuwa katika mgomo, wakauweka kando kwanza kumhudumia Ulimboka. Hapa wanampekeka katika chumba cha mapokezi
 Ushirikiano wa madaktari na wauguzni kuokoa maisha ya Dk. Ulimboka ukawa wa kutosha kama hivi
 Watu wakalizunguka Ambulace iliyomleta Ulimkoka Muhimbili
 Kma hivi
 Madaktari, wauguzi na waandushi wa habari wakiwa katika pilikapilika kujua kwa kuna hatma ya Ulimboka
 Wakasimama  makundi kama hivi
 Polisi wakazidi kuwa karibu na tukio
Huyu jamaa akizungumza na waandishi wa habari. akidai kupigwa na madaktari  eti alishabikia mbele yao kupigwa Ulimboka

0 comments:

Post a Comment