JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu:
255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA
BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dkt. John Pombe Magufuli
leo Ijumaa ya tarehe 09 Desemba, 2016 amewaongoza viongozi mbalimbali na wananchi
kwa ujumla katika maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara .
Maadhimisho
hayo ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara yamefanyika katika uwanja wa Uhuru
Jijini Dar es salaam na kupambwa na gwaride maalum lililoandaliwa kwa pamoja na
Majeshi ya Ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Jeshi la wananchi wa Tanzania
JWTZ,Jeshi la Polisi,Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa.
Akizungumza
na halaiki ya watanzania waliohudhuria sherehe hizo Rais Dkt Magufuli amesema
mwaka jana alilazimika kuzuia kufanyika kwa shamrashamra ya maadhimisho ya
Uhuru wa Tanzania Bara kutimiza miaka 54 kwa kuwa alikuwa na mwezi mmoja tu
tangu aingie madarakani na kuitaja sababu ya pili kuwa ni bajeti kubwa ya shilingi bilioni nne
iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya maadhimiso hayo na kuona ni vyema ikaelekezwa
katika upanuzi wa barabara ya Alli Hassani Mwinyi yenye urefu wa kilomita 4
ambayo inatumiwa na Watanzania wote badala ya fedha zile kutumiwa na wachache.
"Sherehe
za miaka 55 nimeamua zifanyike kwasababu gharama zake ni ndogo sana,kwanza
hakuna hata chakula baada ya sherehe hii,hakuna dhifa ya Taifa ,tukimaliza hapa
tumemalizana ,lakini pili niliamua sherehe hii niifanye hapa Dar es Salaam kwa
kuwa yatakuwa ni maadhimisho ya mwisho kufanyika jijini Dar es salaam na kwamba
ni matumaini yake kuwa sherehe za mwaka kesho zitafanyika makao makuu ya nchia mbayo
ni Dodoma"
Ameongeza
kuwa sherehe za Uhuru ni tukio kubwa sana katika Taifa na hivyo serikali
itaendelea kuipa umuhimu siku hiyo na kuiadhimisha.
Rais
Dkt Magufuli pia amezitaja changamoto ambazo serikali ya awamu ya tano
inazokumbana nazo kuwa ni pamoja na ufisadi na rushwa ndani ya baadhi ya
watendaji na kuongeza kuwa mpaka sasa hivi wafanyakazi hewa wamefikia elfu kumi
na tisa huku kaya masikini hewa zinazonufaika na mfuko wa TASAF zikiwa ni elfu
55 na wanafunzi hewa mpaka sasa hivi
wamefikia elfu sitini na tano
"Serikali
ya awamu ya Tano itaendelea kuchukua hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwatumbua
hadharani wale waliozoea kutumbua hadharani mali za watanzania na tuataendelea
kuchukua hatua kali katika masuala ya rushwa na ufisadi,kwasababu rushwa ni
saratani"
Rais
Dkt Magufuli amepongeza pia jitihada zilizofanywa na watangulizi wake katika
maendeleo ya Tanzania na kuwashukuru kwa niaba ya watanzania huku akiwataka
watanzania wote bila ya kujali dini,itikadi za kisiasa na makabila yao kuendelea kudumisha amani na
mshikamano ili Tanzania iweze kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.
"Hivyo
basi tuendelee kuilinda amani yetu na kuwafichua watu wenye nia ovu ya kuhatarisha
amani yetu na sambamba na kulinda amani yetu hatuna budi kudumisha umoja na
mshikamano wetu ambao ni nguvu na silaha yetu kubwa kama Taifa,lakini pia
tuendelee kuulinda muungano wetu ambao ni silaha kubwa ya umoja wetu ili
Tanzania tuendelee kwenda mbele"
Hii
ni mara ya kwanza kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kuhudhuria na kuhutubia
katika sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara tangu aingie madarakani.
Emmanuel
Buhohela
Kaimu
Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar
es Salaam
09
Desemba, 2016
0 comments:
Post a Comment