TARIME, TANZANIA
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, mjini ya Jaji Amir Mruma imemuhukumu Mkazi wa Tarime Chomete John Wambura kwenda jela miaka tisa baada ya kupatikana na hatia ya kuuwa bila kukusudia.
Katika kesi hiyo, Wambura amepatikana na hatia ya kumuua Chacha Ryoba Mkono kwa kumchoma kisu wakati wa ugomvi wakati wakicheza mchezo wa Pool.
Akitoa Hukumu hiyo Jumanne Wiki hii Jaji Mruma alidai kuwa amelidhika na Ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo bila Shaka yoyote na Mtuhumiwa kuiomba Mahakama imsamehe kwani kosa lake la Kwanza na walikuwa wakigombea sh 200/= wakati wakicheza Pool ,
Ambapo ilidaiwa na Mwanasheria wa Serikali Varence Mayega kuwa Mtuhumiwa Chomete alifanya Mauaji hayo Agost 19/2009 Mchana katika Kijiji cha Genkuru tarafa ya Ingwe alipomchoma Mwenzake Chacha Ryoba Kisu wakati wakigombana na Kusababisha Kifo kwa Ryoba , mbali na Mtuhumiwa kuiomba Mahakama imusamehe kwa kuwa amekaa Mahabusu kwa mda mrefu Jaji Mruma alimuhukumu Kwenda Jela Miaka 9 ili iwe Fundisho kwa watu wengine wanaoondoa Roho za Watu bila Sababu za Msingi ,
Katika kesi nyingine katika Mahakama hiyo Kuu ya Jaji Mruma imemuhukumu Marwa Magembe naye kwenda Jela miaka 9 kwa kuuwa bila kukusudia , ambapo Mwanasheria wa Serikali Mayega alidai kuwa Matuhumiwa Magembe alimuuwa Murian Chacha Tugara usiku Agost 19 /2010 katika Kijiji cha Nyantira Tarafa ya Ingwe
0 comments:
Post a Comment